Akizungumza na jarida letu la THE SUPERSTAR nyota huyo wa miziki wa injili amesema kuwa anafurahia wokovu na kumuimbia Mungu nyimbo za sifa.
Nancy amefichua vile alivyo ingia katika miziki ya dunia aliyompa umaarufu katika mikahawa na vilabu mbali mbali nchini.
Wengi walimfahamu kwa jina Binti wa Subukia hadi wakati alipoamua kuigura sanaa kwa muda mfupi ili kuwaza njia mwafaka.
Nancy KIM sasa amerejea na ujio mkubwa na wa ajabu baada ya kuwachia kibao ambacho kwa sasa kimeenea kwote,mziki ambao anasema kuwa alipata ufunuo kutoka kwa Mungu baada ya kipindi kirefu cha maombi.
Katika album yake mpya aliyofanya kwa lugha ya Agikuyu na ambayo ina nyimbo nne
1.Mururumo wa Jehova
2.Tageria Mahoya
Miongoni mwa vibao vingine abavyo atakuwa anaviweka wazi kwenye launch yake tarehe 13-oct.2019 katika kanisa la K.A.G MERIRONI kaunti ya NAKURU anasema kuwa huu ni ujio mpya usio na njia ya kuzuilika.
Nancy kama wasanii wengine vile vile amezungumzia changamoto si haba katika mziki ikiwemo fedha za kurekodi pamoja na kupenya katika sanaa hii ya mziki.
Wengi wanamuita superstar kwa sauti yake nzuri na bidii yake katika mziki pata kujua mengi kwenye launch yake.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.