Polisi katika eneo la Molo wanaendelea na upelelezi wa jinsi wahalifu wanavyoharibu mataa ya mulika mwizi ili kuweza kuhangaisha wakazi mjini Molo na viunga vyake
Baadhi ya maeneo yamesalia gizani baada ya wahalifu hao kuharibu mataa ya usalama.
Katika eneo la Mutirithia taa iliyokuwa imesalia imeharibiwa usiku wa kuamkia leo huku wakazi wakisema wanahofu huenda wahalifu wakaendelea na visa vya kuvunja nyumba pamoja na maduka na kuiba mali
Mkuu wa polisi kaunti ndogo ya Molo Isaac Odumbe amesema maafisa wa usalama wameimarisha doria haswa nyakati za usiku.
Mca wa Molo Michael Karanja Sonis amesema imekuwa gharama kubwa kufanyia ukarabati taa zilizoharibiwa na wahalifu.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.