Hebu fikiria unapopata fedha unaanza na nini? Kulipa madeni, kulipa bili, kununua vyakula, kununua nguo, kulipia starehe na mapumziko mbalimbali. Baada ya siku chache za kupata fedha unakuwa umeimaliza yote, huku wewe ukibaki mtupu kabisa.
Sasa rafiki, jua kwamba huwezi kuwa huru kifedha kama utaendekeza utaratibu huo wa kuwalipa wengine na kujisahau wewe mwenyewe. Kwenye kila kipato unachoingiza, mtu wa kwanza kumlipa unapaswa kuwa wewe.
Najua hapa huelewi vizuri, kwamba unajilipaje, na hayo matumizi si ndiyo kujilipa? Jibu ni hapana. Na hapa nitakuomba ufanye rejea kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kwenye kipengele cha DHANA YA KUJILIPA WEWE MWENYEWE KWANZA.
Kama mpaka huna kitabu hicho, piga simu au tuma ujumbe kwenda namba 0678 977 007 na utaletewa au kutumiwa kitabu ulipo.
#SomaVitabuTanzania
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.