Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

Mbio za kumkumbuka askofu wa jimbo la Eldoret marehemu Cornelius korir zimezinduliwa rasmi hii Leo

Mbio za kumkumbuka askofu wa jimbo la eldoret marehemu Cornelius korir imezinduliwa rasmi hii Leo na padre mkuu William kosgei.
Akizungumza na wanahabari padre kosgei kwa niaba ya askofu msimamizi wa jimbo hilo la Eldoret Maurice Anthony crawley ametoa mwaliko kwa wananchi kwa ujumla kuweza kujitokeza kushiriki katika mbio hizo za nyika zitakazoandaliwa katika uwanja wa sports club mjini eldoret tarehe 2 mwezi wa kumi na moja Mwaka huu.
Usajili wa mbio hizo vilevile utawajumuisha wanafunzi ambapo kitengo cha kwanza ni wanafunzi wa kati ya miaka 6 na 10, na wale wa miaka kati ya 12-15, wale wa shule za upili wavulana kwa wasichana, timu za parokia wanaume kwa wanawake.
Kwa wale watu tajika katika jamii watahitajika kulipia kima cha shilingi mia tano kwa kila mtu wakti kila kundi likitarajiwa kuwa na watu sita huku parokia zikipewa nafasi kuwa na idadi kubwa.

About KELVIN WILLIAMS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.