Licha ya Mwanariadha Eliud Kipchoge kuvunja
rekodi yake mwenyewe na kuandikisha historia kwa kuwa mwanadamu wa kwanza
kukimbia masafa ya kilomita arubaini na mbili kwa kutumia muda wa saa moja
dakika hamsini na tisa na sekunde arubaini duniani,shirikisho la riadha duniani
IAAF linasema kuwa halitatambua rekodi hiyo.
Kwa
mjibu wa jarida la Game yetu la sharika la The standard,IAAF inasema kuwa sheria
saba za shirikisho hilo zilivunjwa katika riadha hizo.
Baadhi
ya sheria zilizovunjwa kwa mjibu wa IAAF ni kuwa.
1.Wanariadha
wasaidizi maarufu pacemakers,hawafai
kubadilishana kama ilivyoonekana katika mbio hizo za leo.
2.Lazima
kuwe na uchunguzi wa dawa za kusisimua misuli kabla ya shindano lolote,ili hali
halikuwepo.
3.Vinywaji
vinafaa kuchukuliwa katika vituo vilivyoidhinishwa bali sio mwanariadha
kuletewa kama alivyoletewa Kipchoge.
4.Lazima
kuwa na angalau wanariadha watatu wanaoshindana,ili hali Kipchoge hakuwa na
mpinzani hata mmoja.
5.Mwanariadha
hafai kudhibitiwa na gari ambalo lina kidhibiti kama ilivyoonekana katika
hafala ya kipchoge hii leo.
6.
Shindano hilo linafaa kufuatiliwa,kuidhinishwa na kutuzwa na afisa
aliyeidhinishwa na shirikisho la IAAF.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.