Saa chache tu baada ya mshirikishi wa masuala ya serikali
kuu katika iliyokuwa mkoa wa bonde la ufa George Natembeya kuzuru kaunti ya
Baringo na kutangaza vita dhidi ya wezi wa mifugo,kundi moja la wezi waliweza
kuvaamia tena kijiji cha Yatia kwenye eneobunge la Baringo kaskazini usiku wa
kuamkia leo,na kutoweka na mbuzi 33 kuelekea eneo la Che-si-ri-mion kwenye eneobunge
jirani la Tiaty.
Christopher Cherogony ambaye ni mwaadhiriwa wa kisa hicho
cha mavaamizi anasema wezi hao walifika nyumbani kwake mwendo wa saa tano za
usiku,na kufungulia mbuzi wake na kwa kuhofia usalama wake,yeye na familia yake
waliamua kutulia ndani ya nyumba hadi wezi walipoweza kuondoka.
Kisa hicho kimeibua wasiwasi mwingi wa kiusalama katika
eneohilo,huku Richard Chepchome ambaye
ni mkereketwa wa maswala ya amani katika kaunti hiyo akitoa wito kwa serikali
kuendesha operesheni ya dharura katika eneohilo,kama alivyokuwa ameahidi bwana
Natemebeya.
Alipohutubu mjini Kabarnet,Natemebeya aliweza wazi kwamba
serikali inaweka mikakati za kubuni kambi ya kuendesha operesheni katika maeneo
zinazokumbwa na usalama,huku akionya kwamba machifu watabeba msalaba iwapo
mifugo walioibwa watapitishwa katika maeneo yao.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.