Chama
cha wafanyakazi humu nchini tawi la kaunti ya Elgeyo Marakwet limeitaka
serikali ya kaunti hiyo kushugulikia malipo yanayokatwa kutoka kwa mishahara
yao ili kuwaondolea faini na riba kutokana na kuchelewa kulipwa kwa mikopo
kwenye benki.
Pesa
hizo zinazokatwa ni pamoja na zile za kulipia mikopo kwenye benki, bima ya afya
ya matibabu NHIF, hazina ya kusimamia pesa za uzeeni NSSF pamoja na lap
fund.
Wakiongozwa
na katibu wa chama hicho James Kangogo, wafanyakazi hao wamesikitishwa na hatua
ya serikali ya kaunti hiyo ya kuchelewesha malipo hayo ya mwezi wa Julai
kwani huenda ikatatiza shughuli zao za kawaida pamoja na maendeleo ya
kibinafsi.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.