Mratibu
wa kanda ya bonde la ufa George Natembeya ametangaza kufungwa kwa shule
kumi na tano katika msitu Mau ambazo amesema zimekuwa zikihudumu
kiharamu.
Akiongea
afisini mwake mjini Nakuru Natembeya
amesema hii ni mojawapo ya hatua katika awamu ya pili ya kuwaondoa
waliongia msituni humo .Amesema takriban familia elfu kumi zitaathirika
na zoezi hilo.
Kamishna
huyu vilevile amedokeza kuwa serikali inalenga kurejesha ardhi hekari
kumi na saba elfu zilizonyakuliwa kwa jumla ya hekari arobaini na sita
elfu za msitu Mau.
Wakati
uohuo Natembeya amesema kuwa wameanzisha mpango wa kuweka ua wa umeme sawa na
kuongeza alama zinazowekwa kudhihirisha mipaka ya ardhi maarufu beacons
katika juhudi za kuhifadhi msitu huo.
Ameahidi uwepo wa maafisa wa kutosha katika shughuli hiyo nzima.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.