"Mungu ni mwaminifu,ukimwamini na kumtegemea kwakweli hatakuwacha" Ndiyo matamshi ya kwanza kutoka kwa chipukizi huyu wa nyimbo za injili aliyepata fursa hadimu kuzungumza na jarida hili la The Superstar.
Kaka Isaac kama anavyo julikana na wengi katika sanaa yake ya mziki ni kijana aliyezaliwa kutoka familia ya uchochole mjini Kitale katika kijiji cha Matisi.
Anasema kuwa maisha yamemfunza mengi ambayo hakuwa anajua kama angefaulu kuyashinda na kuwa hai leo na vile vile kunawiri katika usanii jinsi alivyo kwa sasa.
Mziki sio rahisi haswa msanii anapokosa usaidizi wa kifedha,mara nyingi wasanii wengi wamekosa kusikika ama kung'aa kwa kukosa fedha za kurekodi miziki yao,lakini kwa Kaka Isaac umaskini na ufukara haukumzuia kuifuata na kutimiza ndoto yake,Anasema "Mimi nililelewa katika jamii fukara iliyotengwa na wote waliotuzunguka,watu walituona kama wasiofaa,maana hatukuwa na pesa wala heshima ,tulitumiwa kama mfano mzuri wa watu waliofeli katika maisha" aliongeza kuwa babake mzazi alipofariki jamii ikawatenga,maisha yakawa magumu sana, walikula kwa kukota na kuomba omba mitaani kutoka kwa wasamaria wema.
Lakini mungu si athumani,wala hamsahau mja wake, maana hakumuawacha Isaac kupitia katika huduma yake wa uimbaji .
Isaac ambaye sasaa amewashangaza wengi amefanya album ya kwanza na anaaminui kuwa na nyingi zaidi.
Nyimbo zake zinapatikana kwa sasa katika YouTube kupitia jina Kaka Isaac
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.