Mwalimu wa shule ya msingi ya Chebore iliyoko katika
eneobunge la Baringo kaskazini ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 300 hii
leo na mahakama ya Kabarnet,baada ya kushtakiwa kwa kosa la kumnajisi mwanafunzi wake wa darasa la saba.
Mshukiwa kwa jina Allan Cheburet kutoka wadi ya Barwessa
alifikishwa mbele ya hakimu mkaazi wa Kabarnet Vienna Ambogo, na kushtakiwa
kwamba mnamo tarehe 31 mwezi uliopita wa saba mwaka huu wa 2019 katika kituo
cha kbiashara cha Barwessa,yeye aliweza kumhadaa mwanafunzi huyo mwenye umri wa
miaka 13,na kumdhulumu kimapenzi mwendo wa saa saba za mchana.
Mshukiwa aliweza kukana shtaka hilo na kuachiliwa kwa
dhamana hiyo ambapo,atatarajiwa kufika mahakamani tarehe 14 mwezi huu wa Agosti
ambapo kesi hiyo itaweza kusikizwa.
Kesi hiyo imewasilishwa siku moja tu baada ya mshtakiwa
mwingine kwa jina David Kipkemoi kuwasilishwa kwenye mahakama jana
Alhamisi,na kushtakiwa kwa kosa la kumnajisi mtoto msichana mwenye umri wa
mwaka mmoja,katika kijiji cha Kaptimbor kilichoko viungani mwa mji wa Kabarnet.
Mshukiwa huyo aliweza kuzuiliwa na kutarajiwa
mahakamani tarehe 13 ambapo kesi yake itasikizwa rasmi.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.