Hamna shughuli zozote zitakazoendelezwa katika msitu wa
Mau kulingana na kamisha kanda ya bonde la ufa George Natembeya .
Akiongea na wanahabari Natembeya amesema kuwa mjadala
kuhusiana na kuondolewa kwa wanaoishi katika msitu huo umezidi kuzua hisia mseto miongoni mwa wananchi jambo
ambalo lazima lishughulikiwe kikamilifu.
Kamishna huyo anasema Serikali kupitia kamati ya watu kumi
inayowahusisha wadau inatarajiwa kuanza shughuli hiyo ya siku sitini
katika eneo la kusini mwa Mau.
Natembeya amesema haya baada ya kikao na wadau hao akidokeza
kuwa serikali vilevile inapanga kuweka ua wa umeme kama njia moja ya kuzuilia
shughuli za kulima na hata kuingiza mifugo kwenye msitu huo.
Vile vile amewarai wanasissa kushirikiana na serikali
kufanikisha mpango huo akikana madai kuwa serikali ilitoa hati
miliki katika ardhi ya msitu ambayo ni vyanzo vya maji nchini.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.