Mbunge wa Gilgil Martha Wangari na Seneta wa kaunti ya Nakuru Susan
Kihika sasa wamesema watapeleka mswada bungeni ili kupunguza faini zinazotozwa
kwa wale wanaofanya makosa madogo.
Wakizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha pesa kwa wachuuzi waliotiwa
nguvuni wiki jana iliyopita katika eneo la kupima uzani wa magari la Gilgil,
wawili hao wamesema kuwa sheria ya sasa ilikuwa finyu kwa wale wenye makosa
yasiyofaa kifungo cha jela.
Kulingana na Wangari hatua ya kushikwa na kufikishwa mahakamani kwa wachuuzi
hao baada ya kuondolewa kwa lazima eneo hilo na shirika la kusimamia barabara
za kitaifa haikufaa hata kidogo.
Mbunge huyo amesema wachuuzi hao walikuwa wakitafuta lishe kwa familia
zao kwa kuuza bidhaa kama vile maji na walifaa kusaidiwa badala ya kuwaondoa.
Naye Kihika amekemea hatua hiyo na kusema wachuuzi hao walitozwa faini
ambazo hawawezi kuzikimu kwani wengi ni maskini wanaoishi katika vitongoji duni
vya Gilgil.
Wengine waliozungumza ni pamoja na mwakilishi wa wadi ya Giglil Jane
Ngugi na viongozi wengine wa mji huo.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.