Wanafunzi wapatao 500 wa chuo kikuu cha Moi wameandamana
baada ya majina yao kukosa kwenye orodha ya watakaofuzu wakiilaumu
usimamizi wa chuo hicho kwa kutoshughulikia swala hilo.
Wanafunzi
hao waliopiga kambi kwenye chuo hicho, wamesema kuwa
wamekuwa wakipitia changamoto kwa miaka mingi bila usimamizi wa
chuo hicho kutafuta suluhu.
Wamedai
kuwa, baadhi yao wangekuwa wamefuzu miaka miwili ama tatu zilizopita
lakini chuo hicho kimekuwa kikihairisha wakati wao wakuhitimu huku
wakiongezea kuwa, wakati mmoja wanaosimamia usalama chuoni humo
waliwafurusha nje ya chuo hicho.
Sasa
wanataka majina yao yajumuishwe na ya wanafunzi wengine watakaofuzu
mwezi huu la sivyo, watafika mahakamani kusimamisha sherehe ya kufuzu
inayotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 22/08/2019.
Juhudi za kuwafikia wasimamizi wa chuo hicho cha Moi ziligonga mwamba.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.