Idara ya afya na usafi wa umma imesema kuwa itaizika takriban miili 25
katika kaburi la umma mjini Naivasha baada ya kupata idhini la mahakama.
Miili hiyo imekuwa kwenye hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya kaunti
ndogo ya Naivasha kwa zaidi ya miezi sita bila ya kuchukuliwa.
Kulingana na mkuu
msimamizi wa hospitali hiyo Dkt Angeline Ithondeka, hatua hiyo itapelekea wao
kupunguza fedha wanazotumia kuifadhi miili hiyo hospitalini.
Ithondeka amesema
miili hiyo na ambayo itazikwa katika makaburi ya umma huko Longonot ililetwa
kutoka sehemu tofauti huku ile mingi ikiwa ya wahanga wa ajali zinazotokea
kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nairobi, Mai Mahiu kuelekea Naivasha na
Mai Mahiu kielekea Narok.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.