Shughuli za usafiri
kwenye barabara kuu ya kuelekea kusini mwa ziwa la Naivasha zimekwama kwa siku
ya pili mfululizo baada ya wakazi wa maeneo ya karagita, Kamere, DCK, Kwa Muhia
na Kongoni kuifunga wakitaka ikarabatiwe.
Wengi waliokuwa
wakielekea kazini hususan katika mashamba ya maua hawakufanya hivyo huku
barabara hiyo ikifungwa mapema kwa mawe na kuchomwa kwa magurudumu ya magari.
Aidha juhudi za polisi
zwa kuzima ghasia za kujaribu kurejesha hali ya kawaida hazikufua dafu kwani
walizidiwa na wakazi waliojawa na hasira licha ya hata kuwatupia vitoa machozi
na kufyatua risasi kadhaa hewani.
Mkazi mmoja Amos Kimani
amesema wataendelea kuifunga barabara hiyo na kuhalalisha shughuli za usafiri
hadi pale serikali itaamua kuitengeneza upya.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.