Serikali sasa imelegeza kamba na kusema kuwa barabara inayoelekea kusini
mwa ziwa la Naivasha itakarabatiwa upya huku mwanakandarasi akitumwa katika
kipindi cha wiki tatu zijazo.
Hii ni kufuatia maandamano ya wakazi ya siku mbili mfululizo huku
shughuli za kawaida zikihalalishwa na wafanyibiashara wengi kukadiria hasara
kubwa.
Huku akikiri kuwa mgomo huo uliadhiri pakubwa huduma muhimu, naibu wa
kamishan wa kaunti ndogo ya Naivasha Mbogo Mathioya amesema mwanakandarasi huyo
atafika mnamo tarehe 15 mwezi ujao tayari kuanza kazi hiyo.
Haya yamejiri huku zaidi ya wafanyikazi 5,000 wakikosa kufika kazini
katika maeneo ya Olkaria na kampuni za maua huku waajiri hao wakisema mgomo
uliokuwepo ulileta madhara makubwa.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.