Takriban wahudumu mia mbili wa sekta ya utalii barani Afrika wanatarajiwa
kukongamana mjini Naivasha ili kujadili maswala ibuka ya sekta hiyo na ambayo
inakabiliwa na changa moto si haba.
Mkutano huo utalenga kuangalia madhara yatakayolewa na kuanguka kwa
kampuni ya kimataifa ya Thomas Cook ambayo huwaleta watalii kutoka bara Uropa
hadi Afrika na pia kuangalia mbini mbadala ya kuwafikia watalii katika bara
zingine.
Akizungumza na kituo hiki kabla ya kuanza kwa mkutano huo, mkurugenzi
mkuu wa shirika la wahudumu wa sekta ya utalii KATA Nicanor Sabula amesema kuwa kongamano hilo litajadili kwa
mapana sekta hiyo na kuona jinsi ya kuipanua kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Mnamo Jumatatu wiki hii, kampuni ya
Thomas Cook ilitangaza kumaliza biashara hiyo na kuwaadhiri maelfu ya watalii
kutoka Uropa waliokuwa tayari wamelipa nauli za ndege kusafiri sehemu tofauti
ulimwenguni.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.