Wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Nakuru wamesema baadhi ya maafisa
wakuu wa serikali ya kitaifa wameanza kuwapa vitisho ili kuweza kuangusha
mswada wa Ekuru Aukot wa Punguza mzigo unaolenga kubadilisha katiba ili kuondoa
nyadhifa Fulani.
Haya yamejiri huku wawakilishi hao wakiitwa kwa mkutano katika hoteli
moja mjini Naivasha na kuarifiwa madhara ya mswada huo huku kikao na wanahabari
walichokuwa wamepanga kikikosa kufanyika kwa dakika ya mwisho.
Wengi waliozungumza na kituo hiki japo hawakutaka kutajwa majina yao
wamesema wanashurutishwa kuangusha mswada huo huku wakiletewa watu waliojitaja
kama wataalamu wa maswala ya katiba ili kuambiwa madhara hayo.
Hata hivyo aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hiyo
Stanley Karanja amesema kuwa mkutano huo umejadili maswala mengi yakiwemo yale
ya mikopo ya magari yao na malipo ya uzeeni kwa wafanyikazi wa serikali hiyo
kati ya maswala mengine.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.