Mbunge wa Giglil Martha Wangari sasa amemtaka aliyekuwa mumewe Peter
Karanja kusimamishwa kutowaona watoto wao wawili kutokana na kesi inayomkabili
kwa sasa.
Kwenye maombi yaliyowasilishwa mahakamani na wakili wa mbunge huyo George
Kimani, Wangari amesema watoto wao wanakumbana na matatizo ya kiakili baada ya
kuona baba yao alikuwa na kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Tob Cohen.
Wangari aidha ameitaka mahakama hiyo kumshurutisha Karanja kilipa
shilingi 270,000 za kushughulikia mahitaji ya watoto wao wawili pamoja na
kulipa karo za shule.
Huku akifika mbele ya hakimu mkuu wa Naivasha Joseph Karanja, mbunge huyo
amesema mumewe wa zamani asiruhusiwe kuwaona watoto wake hadi pale kesi
inayomkabili itasikiziwa na kukamilishwa.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.