Mbiwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Karagita mjini Naivasha
baada ya mwanamume mmoja kujitoa uhai kwa kutambuwa mkewe alipachikwa mimba na
rafiki wake wa karibu.
Wengi wa wakazi wa kitongoji duni hicho walipatwa na butwaa baada ya
kutazama kilichokuwa kikiendelea huku wakisema kuwa mwendazake na ambaye
alikuwa mfanyikazi wa kampuni moja ya maua alikuwa mtulivu na mfupi wa maneno.
Kulingana na jirani yake tuliyemtambua tu kwa jina Ouma, mwendazake
alikuwa na marafiki wake wakati alipashwa habari kuhusu mimba ya mkewe na
alipofika nyumbani akamuuliza mkewe na ambaye alidhibitisha taarifa kuwa mimba
hiyo haikuwa yake.
OCPD wa Naivasha Samuel Waweru amedhibitisha tukio hilo na kusema mwili
huo umechukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali
kuu ya kaunti ndogo ya Naivasha.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.