Kulikuwa na hali ya hofu katika kijiji cha Kinamba mjini Naivasha baada
ya mwanamume mmoja na ambaye ni baba wa watoto watano kujitoa uhai kwa
kujinyonga.
Mwili wa mwendazake umepatikana hii leo na wakazi waliokuwa wakielekea
kazini huku polisi wakifika na kuuchukua mwili huo.
Kulingana na mkazi mmoja John Mbugua, mwendazake amekuwa akiugua kwa muda
mrefu na aliwaarifu marafiki wake alichokuwa akipania kufanya baada ya
kutambuwa kuwa ugonjwa aliokuwa nao haungepona.
OCPD wa Naivasha Samuel Waweru amedhibitisha tukio hilo na kusema mwili
huo umechukuliwa na kupelekwa katika mochari ya hospitali kuu ya kaunti ndogo
ya Naivasha ukisubiri kufanyiwa upasuaji.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.