Ni kweli dunia nzima imekuwa ikiwakashifu wananwake kwa maswala ya ukahaba na anasa,lakini swali kuu ni kuwa JE?Wanafanya ukahaba na nani kama sio wanaume?
Mwanamke ni kiumbe ambacho kilipewa moyo wa huruma na moyo wa kujali,wakati mwanamke mdogo anaporingwa miba na mwanamme kisha mwanamme huyo anakwepa majukumu ilihali msicha huyo pia amekataliwa na wazazi kwa kuwapa aibu,huwa anatafuta mbinu ya kujistahimili katika maisha.
Msichana huyu mara nyingi unapata kuwa bado hana kazi wala hajawai kujitegemea kwa maisha,bado hana tajriba yoyote ilihali tayari ameingia katika majukumu ya malezi.
Kulea mimba ni gharama ya juu,kuzaa mtoto ni gharama na sasa pia kumlea mtoto huyo ni gharama nyingine,lakini baba ya huyo mtoto hajulikani alipo na wala hajali kama ana mtoto yeyote.
Asilimia kubwa ya wanawake wamejipata katika hali hii ndiposa wakaamua kutafuta mbinu yoyote ile ya kujisitiri katika maisha.
Kufuatia msukumo wa kukabiliana na hali hii,wanawake wanajipata mikononi mwa wanaume wawa hawa,sasa wanaojifanya kuwafariji kwa kuwapa hela kadhaa za matumizi kwa kuhurumia hali wanayopita.
Lakini kila mwanamme huingia katika maisha ya mwanamke na sababu zake binafsi ambazo ni vigumu saana kwa mwanamee kujua.
Ni hulka ya mwanamke kupendezwa na mambo anayoona kwa macho kuliko ukweli ambao haujadhihirika.
Hivyo basi licha ya matatizo ambayo mwanamke huyu anapitia,ujanja wa mwanamme bado unamzidi na anajipata katika mikono ya mlaji tu ila sio mtunzi.
Wanawake ambao wamepewa mimba na wakatelekezwa na wanaume ndio hujipata kwenye mikono ya wanaume hawa wakora,wanaotaka tu kuwatumia kimapenzi na kisha kuwaaacha.
Lakini kwa sasabu ya shida na vilevile gharama za kumlea mtoto,kando na ukosefu wa kazi nchini,wasichana hawa wanakubali vipesa vidogo wanavyo pewa na wanaume hawa na hivyo ndivyo sasa ukahaba unaanza.
Mwanamke ataishi kwa kupeana mwili wake ili kusaidia mtoto ambaye hana hatia na hafai kuangamia kwa makosa ya wazazi.
Ukweli mchungu ni kuwa iwapo wanaume watakubali majukumu yao basi idadi ya wananwake wanaojihusisha na anasa itapungua kwa kiwango kikubwa.
Wakati wa wanaume kuamka na kuchukulia majukumu yao kwa kumaanisha umefika
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.