Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

Polisi huko Gilgil wanamsaka mwanamume mmoja ambaye alimuua kwa kumkata mkewe akitumia panga baada ya kumshuku alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake.

Polisi huko Gilgil wanamsaka mwanamume mmoja ambaye alimuua kwa kumkata mkewe akitumia panga baada ya kumshuku alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake.
Wakati wa tukio hilo katika eneo la Kambi Turkana wadi ya Eburru/Mbaruk, mshukiwa huyo anadaiwa kumkata mkewe wa watoto saba huku kitinda mimba wao akitazama.
Jirani wao Jane Adomeniti amesema kuwa walisikia nduru kutoka kwa makazi ya familia hiyo na walipofika wakapata tayari mwendazake amekata roho.
Aidha mbiwi la simanzi lilitanda kote eneo hilo huku wakazi wakijaribu kutadhmini mauti yaliyowakumba kwa jirani waliomjua kwa miaka mingi.
OCPD wa Gilgil Emmanuel Opuru amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa kiini cha mauaji hayo hakijabainika japokuwa walikuwa wakimsaka mwanamume huyo na ambaye ni mshukiwa mkuu ili afunguliwe mashtaka.

About KELVIN WILLIAMS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.