Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

Tume ya kuwaajiri waalimu nchini TSC imewaondoa waalimu wapatao 72,000 kutoka kwa orodha ya muungano wa waalimu wa KNUT

Tume ya kuwaajiri waalimu nchini TSC imewaondoa waalimu wapatao 72,000 kutoka kwa orodha ya muungano wa waalimu wa KNUT.

Jarida moja la hapa nchini linasema baada ya mahakama ya leba kuishurutisha TSC kusalimisha kwa KNUT pesa inazokata waalimu, TSC ilikata kiasi cha milioni 83 kutoka kwa waalimu  115,000.
Hapo awali Knut ilikuwa na wanachama wapatao 187,000 waliokuwa wakichangia muungani huo hadi kiasi cha shilingi milioni 140 kila mwezi. 

Hii ina maanisha kwamba kwa mwezi wa septemba pekee, KNUT imepoteza jumla ya shilingi milioni 57.
Kutokana na mkanganyo huo, KNUT imeripotiwa kufanya mkutano wa udharura hiyo jana kujadili swala hilo, huku fedha walizostahili kupokea katika miezi ya Julai na Agosti zikiendelea kuibua sintofahamu.
Hata hivyo katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion anasema muungano huo unafanya mazungumzo na TSC.

About KELVIN WILLIAMS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.