Spika wa bunge la seneti Kenneth Lusaka amesema ataendelea
kuandamana na naibu wa rais William Samoei Ruto katika ziara zake mbali mbali
nchini.
Lusaka ametetea uwepo wake katika ziara za kisiasa na
michango ya naibu rais haswa Magharibi mwa Kenya akisema yeye hufanya hivyo
kama afisa wa serikali ila sio kama mfuasi wa dkt William Ruto.
Akiongea na jarida moja la hapa nchini, Lusaka amesema uwepo
wake katika mikutano ya Ruto hauadhiri kwa vyovyote utendakazi wake kama spika
wa bunge la seneti.
Lusaka alikuwa akirejelea madai ya baadhi ya wanasiasa kwamba
uwepo wake katika mikutano hiyo unaliweka kwenye njia panda bunge la seneti.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.