Afisa wa zamani wa polisi amepatikana na hatia ya kuua afisa
wa mauazo kutokana na mzozo wa kimapenzi, na kufungwa miaka sita gerezani.
Leonard Kanari amepatikana na hatia ya kumuua Christopher
Muganda katika eneo la Kasarani kaunti ya Nairobi mwakani wa 2016.
Wakati akitoa hukumu hiyo, jaji Jesse Lessit amesema Kanari alitumia nguvu zaidi wakati alimpiga
risasi marehemu ambaye hakuwa amejihami.
Kanari anadaiwa kutekeleza hatia hiyo katika mtaa wa Garden
kule Kasarani usiku wa May 26 mwaka
2016.
Kulingana na Eddah Kamau aliyekuwa kwenye utandabui wa
mapenzi hayo ameambia mahakama kwamba
alikuwa mpenzi wa Muganda tangia 2008 na wakabarikiwa na motto msichana.
Jaji Lessit alikanusha
madai ya mshukiwa Kanari kwamba alikuwa akijilinda kutokana na kushambuliwa na
Muganda, ila akasema alimuua baada ya kumpata
katika nyumba ya Eddah.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.