Mwanamme aliyeweka picha na video za utupu wa msichana
aliyekuwa mpenziwe kwenye mitandao ya kijamii, amefikishwa mahakamani kwa kuendeleza dhulma
mitandaoni.
Akiwa mbele ya hakimu mkuu mkaazi Martin Rabera mshukiwa Omar
Seif amekanusha mashtaka na kuachiliwa kwa bondi ya 100,000.
Hii ni baada ya Seif kufahamisha mahakama kwamba ana uchungu
unaomlazimisha kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Mpeketoni kaunti ya
Lamu.
Kundi la kutetea haki za kibinadamu la Sisters for Justice
kupitia mkurugenzi wake mkuu Naila Abdhalla, lilisema mahakamani kwamba visa
vya dhulma mitandaoni vinaongezeka sana kiasi cha waadhiriwa kuamua kujitoa
uhai.
Abdalla anasema licha ya ongezeko hilo haswa miongoni mwa
wanafunzi wa vyuo vikuu, watu wengi wanaogopa kuripoti wamedhulumiwa mitandaoni
kwa kuogopa familia isijue.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.