Familia zinazoishi eneo la Kedong
mjini Naivasha zimeanza kuondoka eneo hilo ili kutwaa nafasi kwa ujenzi wa
miradi ya mvuke.
Hii ni kufuatia agizo la wao
kuondoka eneo hilo na kamati ya usalama ya kaunti ndogo ya Naivasha baada ya
kampuni ya kuendeleza mvuke ya Akira kununua ardhi hiyo yenye ekari elfu moja
ili iweze kufanya mradi huo utakaogharimu shilingi bilioni tisa.
Akidhibitisha taarifa hiyo naibu
kamishna wa kaunti ndogo ya Naivasha Mbogo Mathioya amesema nyingi ya familia
hizo zimeondoka, na walio salia wanatarajiwa
kuondoka katika kipindi cha siku mbili zijazo.
Akizungumza na wanahabari mjini
Naivasha leo hii, Mathioya vile vile amesema familia 23 zilizokuwa zikiishi
kwenye ardhi hiyo zilipewa ekari tano kila moja lakini kumekuwa na ongezeko la
watu na ambao kwa sasa wanaondolewa.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.