Hali ya upungufu wa
maji umeghubikia wakazi wa maeneo ya Eburru, Morgan, Kongasi, Nagum na Gema kaunti
ndogo ya Gilgil baada ya bwawa la Thome lililokuwa likiwapa maji kupasua kingo
zake na kumwaga maji.
Viongozi eneo hilo
wakiongozwa na kiongozi wa wanawake Lydia Nyota wameelekezea kidole cha lawama
kwa mwanakandarasi aliyepewa kazi ya kukarabati bwawa hilo kwa utepetevu
kazini.
Nyota amesema japokuwa
eneo hilo halikuwa na mvua wakati wa mkasa huo haijabainika kilichofanyika na
mwanakandarasi huyo na kupelekea tatizo hilo kufanyika.
Hata hivyo naibu wa
kamishna wa kaunti ndogo ya Giglil Mutheki Ndambuki amedhibitisha tukio hilo na
kusema wahandisi kutoka serikali ya kaunti ya Nakuru wametumwa kuangalia hali
ya sasa ya bwawa hilo japokuwa hakuna aliyejeruhiwa.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.