Serikali ya kaunti ya Nakuru imeanza mpango wa kuchukua ardhi
zilizokuwa zimenyakuliwa na watu waliokuwa na usemi mkubwa serikali za awali.
Akizungumza baada ya kuzuru mji wa Naivasha kukagua miradi ya
maendeleona kuanzisha mradi wa ujenzi wa soko la kisasa la mji huo, Gavana Lee
Kinyanjui amesema amebuni kamati itakayo chunguza ardhi hizo na kutoa ripoti
kikamilifu kabla ya kutekeleza agizo hilo.
Kulingana naye, imekuwa vigumu kutekeleza miradi ya serikali
kwani maeneo wanayokisia kufanya hivyo yamenyakuliwa na watu wanaodai kuwa na
hati miliki ya ardhi ili wafidiwe tukio ambalo amesema ni kinyume cha sheria.
Vile vile Kinyanjui ametoa ilani kwa wanakandarasi
wanaochelewesha miradi waliyopewa kufanya kuwa wataachishwa kazi hiyo iwapo
watapatikana kuwa wana uzembefu kumaliza miradi waliyopewa.
About KELVIN WILLIAMS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.