Gavana wa Baringo Stanley Kiptis na mwenzake wa Pokot
Magharibi John Lonyangapuo wameanzisha juhudi za kurejesha amani katika bonde
la Kerio,na kuhimiza jamii zote za wafugaji kuungana na kuleta maendeleo.
Wakizungumza jana katika eneo la Kolowa kwenye eneobunge la
Tiaty,Gavana Kiptis anasema viongozi wa maeneo zinazokumbwa na tatizo la utovu
wa usalama wana jukumu la kuzungumza kwa sauti moja,na kupinga vitendo
vinavyohujumu maendeleo.
Kiptis anahimiza ujumbe wa amani kusambazwa hadi
mashuleni,huku akihimiza serikali kuu na wadau wengine wa maendeleo kubadilisha
fikira kuhusu ukanda mwa kaskazini mwa bonde la ufa kama eneo hatari.
Aliyekuwa mbunge wa Tiaty Asman Kamama,seneta Kipchumba
Murkomen,mbunge wa Kapseret Oscar Sudi miongoni mwa wengine waliweza kuhudhuria
kikao hicho cha amani.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.