Mshirikishi wa masuala ya serikali kuu katika eneo la bonde la ufa Goerge Natembeya ametangaza vita vikali dhidi ya wezi wa mifugo
ambao wanazidi kutatiza usalama katika eneo la Baringo kwa kuiba mifugo.
Akihutubu mjini Kabarnet ambapo aliweza kukutana na wakuu wa
usalama kwenye kaunti hiyo,Natembeya ameapa hadharani kwamba serikali iko
tayari kuwakabili wezi wa mifugo katika eneo la Baringo,Samburu,Laikipia na pia
Turkana,akaelekeza wakuu wa kaunti hizo kubuni mwongozo wa kuendesha operesheni
hiyo haraka iwezekanavyo.
Wakati huo huo ,Natembeya ametoa makataa ya hadi jumamosi kwa machifu
kurejesha ngombe 55 waliobiwa hivi karibuni kutoka eneobunge la Baringo
kaskazini,huku akionya kwamba machifu watapoteza mifugo wao iwapo watakosa
kushirikiana na serikali kukabili tatizo hilo la wizi.
Natembeya ametangaza msimamo huu wakati ambapo waadhiriwa wa
utovu wa usalama katika maeneo ya Marigat na Baringo kaskazini wanaonekana
kupoteza matumaini ya kuishi kwa amani,kufuatia msururu wa mashambulizi kutoka
kwa wezi wa mifugo ambao wameponekana kupata nguvu mpya,baada ya serikali
kutwaa bunduki zilizokua zikitumika kutoa ulinzi kwa wananchi na mali yao,kupitia
kwa askari wa akiba NPR.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.