Mwili wa mwanafunzi mmoja wa kike wa
kidato cha pili umepatikana kitandani mwake katika kijiji cha Limuru wadi ya
Waseges kaunti ndogo ya Subukia, ukiwa na dalili za kunyongwa na anayekisiwa
kuwa mpenziwe marehemu.
Marehemu ni mwanafunzi katika shule
ya upili ya Keriko na mshukiwa anadaiwa kutekeleza kitendo hicho wakati mvua
ikinyesha, na kisha kutoroka muda mfupi baadaye.
Akidhibitisha tukio hilo mwakilishi
wadi hiyo Daniel Kiriethe Ndigirigi, ametoa wito kwa maafisa wa polisi kusaidia
kwa kupeleka mbwa wa kunusa katika eneo la mkasa, ili kumnasa mtuhumiwa ambaye
amekwenda mafichoni.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.