![]() |
Shirika la Kengen linasema limedhibiti tatizo
lililokuwepo wakati mashine moja ya kutoa kawi ya mvuke ililipuka na kuwaumia
wafanyikazi tisa katika eneo la Olkaria mjini Naivasha.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, mkurugenzi mkuu wa
shirika hilo Rebecca Miano amesema kuwa mashine hiyo ilikuwa ikikaguliwa kabla
ya kawi iliyokuwa ikitoa iunganishwe na gridi ya kitaifa na kuongeza kuwa hatua
hiyo imerekebishwa.
Miano aidha amesema kuwa mashine hiyo ilikuwa ikiangaliwa
ili iweze kuongea kawi inayotoa kutoka megawati 43 hadi megawati 65 wakati wa
tukio hilo na vile vile kusema walikuwa wamejitolea ili kuhakikisha kuwa azimio
lao la kupata takriban megawati 165 katika kipindi cha miaka miwili itatimia.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.