Baadhi ya viongozi pamoja na wakulima wa miwa kwenye kaunti ya Bungoma sasa wanataka kampuni ya kusaga miwa ya Nzoia kubuni bodi mpya ili kufufua shughuli katika kampuni hiyo na kuangazia utumizi mbaya wa fedha na raslimali.
Kwa
mjibu wa jarida moja la humu nchini wanabodi wa sasa wamelaumiwa kwa tuhuma za
kufuja pesa za kampuni hiyo bila kuangazia hasara.
Inaarifiwa
kuwa chini ya mwenyekiti wa bodi hiyo Joash Wamang’oli,wanabodi hukutana mara
tatu kwa mwezi huku shilingi takribani milioni 5 zikitumika katika marupurupu ya
vikao hivyo kutoka kwenye akaunti ya kampuni hiyo.
Gavana
wa Bungoma Whycliffe Wangamati pamoja na mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi
wanadaiwa kuanzisha mikakati ya kubandua bodi hiyo ili kuinusuru kampuni hiyo.
Bodi
hiyo hivi maajuzi ilimteua Michael Makokha kama meneja mkurugenzi kufuatia kifo
cha Michael Kulundu aliyekuwa akihudumu katika wadhifa huo.
Hata
hivyo Makoha amemlaumu Wamunyinyi huku akisema kuwa amekuwa na nia ya
kumuharibia sifa na kung’atua kutoka uongozini bila sababu mahususi.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.