Wanaharakati
wakiongozwa na Suba Churchil sasa wanataka idara ya jinai kumtia mbaroni na
kumzuilia tena gavana wa kiambu Ferdinand Waititu kwa kukiuka maagizo ya
mahakama baada ya kuwachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 15 juma lilipita.
Wamemkashifu
gavana huyo kwa ziara yake wikendi kwenye
maeneo ambayo miradi anayohusishwa nayo katika kesi ya ufisadi na utumizi mbaya
wa mamlaka inatekelezwa kando na
kuhutubia halaiki ya watu.
Wanasema
kuwa hatua hiyo ni kuhitalifiana na ushahidi dhidi ya kesi inayomwandama.
Hata
hivyo gavana huyo amekinzana na wanaharakati hao huku akitaja kuwa bado yuko na mamlaka ya utendakazi kama gavana licha ya
kuwekewa ilani ya kutofika afisini mwake.
Anasema
kuwa mamlaka yake hayako afisini wala kwa gari lake la serikali na hivyo
atazidi kuwahudumia wananchi licha ya kukosa afisi.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.