Hofu imetanda katika eneo la Kiwanjani kaunti ya Isiolo baada ya kilipuzi kupatikana
nje ya afisi ya mwakilishi wa kina mama kaunti hiyo Jaldesa Rehema Dida.
Aidha Kwa mjibu wa idara ya usalama eneo hilo kupitia sajenti wa polisi Peter Ogolla kutoka Laikipia,kifaa hicho ni mabaki ya
kilipuzi na haina hatari yoyote kwa wakaazi na wafanyakazi wa afisi hiyo.
Akizungumza na runinga ya NTV amesema “Ile
kitu imepatikana hapa ni grenade ambayo ilikuwa imekaa kwa muda. Hata
nikiangalia safety pin yake ilikuwa imetoka na ni ya practice. Ya practice
hukuwa na little explosive ndani,”.
Wakaazi sasa wamehimiza maafisa wa usalama kuimarisha doria
katika eneo hilo.
Kifaa hiho kilitambuliwa na wakaazi waliokuwa katika
shughuli zao za kila siku.
Hadi kufikia sasa mwakilishi wa kina mama huyo hajatoa tamko
lolote kuhusiana na kisa hicho
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.