Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

NAIROBI-Mahakama ya upeo imetupulia mbali kesi inayopinga uchaguzi wa Gavana Anne Mumbi Waiganjo

 
Picha- Hisani

Mahakama ya upeo imetupulia mbali  kesi inayopinga uchaguzi wa gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru iliyokuwa imewasilishwa na kinara wa chama cha Nark Kenya Martha Karua.
Katika uamuzi uliosomwa na jaji Isack Lenaola ,mahakama hiyo imesema kuwa Karua hakuwa na sababu za kutosha kubatilisha ushindi gavana Waiguru.
Hata hivyo kinyume na kesi zingine za awali mahakama imewataka wawili hao kwa pamoja kugharamia kesi hiyo.
Akizungumza baada ya uamuzi huo Waiguru ameipongeza mahakama huku akisema kwa sasa ni wakati wa kuwahudumia wakazi wa Kirinyaga na kumtaka Karua kuungana naye katika kufanikisha hilo.
Kauli ambayo imeungwa mkono na naibu gavana Peter Ndambiri.

About VANTAGE MUSIC RECORDS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.