Gavana
wa Kisumu Prof.Peter Anyang’ Nyong’o amelaumiwa
na wakaazi wa kaunti hiyo kufuatia utumizi mbaya wa pesa za umma.
Hii
ni baada ya kubainika kuwa kaunti hiyo ilinunua gari kuu aina ya Toyota Prado
kwa kima cha shilingi milioni 19.
Kwa
mjibu wa taarifa za jarida la Citizen weekly
wawakilishi katika kaunti hiyo vile vile
wanahusishwa na kandarasi zinazotolewa huku ikibainika kuwa wanamiliki kampuni
zinazotekeleza baadhi ya miradi kwenye kaunti huyo.
Wa
hivi karibuni kukashifiwa ni mwakilishi wa wadi ya Railways David Arao amabye anadaiwa kujenga choo katika eneo la bandari
ya Lwang’ni kwa kima cha shilingi milioni 5.
Choo
hicho hata hivyo kimebomolewa kufuatia ukarabati wa bandari hiyo.
Vile
vile kuna baadhi ya viongozi wanaokisiwa kupanga mikakati ya kuvuna fedha za umma
katika mradi wa kuboresha jiji hilo la Kisumu ,mradi unaofadhiliwa na banki ya dunia.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.