Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

NAIROBI-Hongo ya shilingi 1500/- yamtia afisa wa trafiki matatani Nairobi



Afisa mmoja wa trafiki anachunguzwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video akiomba rushwa ya shilingi 1500/- kutoka kwa dereva wa taxi mtaani Eastleigh jijini Nairobi.
Katika kanda ya video iliyosambazwa mtandaoni dereva huyo ambaye hajatambulishwa anasikika akimrai afisa huyo kumuonea huruma kwa kukosa fedha hizo huku akisema hana,na itabidi aombe ndiposa  apate hela hizo.
Afisa huyo aidha anasikikika akisema “Si ulikua unasema uko na elfu moja. Kwa hivo haukua nayo ni kuomba ulikua unaomba yote?
Hata hivyoo dereva huyo alilazimika kumpa afisa huyo fedha hizo kwa mjibu wa video hiyo.
Mamlaka ya Huduma za polisi NPS imethibitisha kupokea kesi hiyo na kuahidi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya afisa huyo.
Tukio hilo linatokea saa chache tu baada ya maafisa wa jinai kumkamata afisa mwengine wa polisi mwenye hadhi ya constable kwa jina Samuel Mutachi kutoka kituo cha polisi cha central jijini Nairobi kwa tuhuma za kuomba hongo ya shilingi elfu 200.
Mutachi aidha alipewa shilingi elfu 35 pekee kutoka kwa wakili mmoja huku akijifanya afisa wa jinai anayechunguza kesi ya kughushi stkabadhi.
Idara ya jinai sasa imewataka wananchi kuwa makini na matapeli wanaojifanya maafisa wa serikali.

About VANTAGE MUSIC RECORDS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.