Watu wawili ambao ni wapendanao wanapigania maisha yao katika hospitali
kuu ya kaunti ndogo ya Naivasha baada ya kujaribu kujiua usiku wa kuamkia leo.
Hii ni kufuatia ripoti zilizowapata kuwa wawili hao walikuwa mabinanu na
hakuna vile wangeoana tukio lililomlazimisha mwanamume kuchukua kisu na
kumdunga mpenziwe kabla ya kujigeukia na kujidunga mwilini.
Hata hivyo njama yao ilitupuka huku majirani wakiitwa na kuwakimbiza
katika hospitali hiyo na kulazwa katika chumba cha wagonjwa wa hali mahututi.
Kulingana na msimamizi wa hospitali hiyo Dkt Angeline Ithondeka, mwanamke
huyo alipata majeraha mabaya kwenye tumbo lake huku mwanamume akiwa na majeraha
ya kufua na wanaendelea kutibiwa.
Chifu wa eneo la Murungaru kulitokotokea kisa hicho Joseph Kimani
amedhibitisha tukio hilo na kusema mwanamume huyo alikuwa akiishi eneo la
Laikipia kabla ya kufika nyumbani kwa kina msichana huyo na kuanza kutekeleza
uovu huo huku akisema hangeishi maisha bila ya mpenziwe.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.