Wakulima wa viazi katika kaunti ya Nyandarua sasa wametaka wenzao kutoka
kaunti zingine kuanza kutekeleza sheria mpya ya kupakia viazi kwenye magunia ya
kilo hamsini.
Kulingana na mkurugenzi wa bodi ya kiwanda cha Midlands kilichoko eneo la
Njambini huko Kinangop Matheri Wahungu, wakulima walioanza kutekeleza sheria
hiyo wanakadiria hasara kwani mazao yao hayanunuliwi kwenye soko.
Wahungu anasema kuwa hatua ya utekelezaji wa sheria hiyo utapelekea wakulima wengi
kunufaika na jasho lao hususan msimu huu ambapo viazi zinapatikana kwa wingi.
Akizungumza na wanahabri mjini Naivasha, mkurugenzi huyo aidha amesema
serikali ya kitaifa ilifaa kusaidiana na zile za kaunti zinazokuza viazi ili
kuona kuwa wakulima wamepata faida ya zao hilo kama njia moja ya kuboresha ukulima
huo.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.