Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

Serikali kuu na ile ya kaunti ya Nakuru kutenga shilingi milioni 90 kwa kilimo cha Pareto



Wizara ya kilimo imeanzisha mpango wa kupanua ardhi zinazolimwa pareto nchini kutoka ekari elfu sita hadi ekari elfu kumi na nane katika muda wa mwaka mmoja ujao.

Akizungumza wakati wa siku ya wakulima  eneo la Eburru kaunti ndogo ya Gilgil, waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri amesema kuwa kupanuliwa huko kutawezesha kenya kuzalisha tani elfu kumi na nane za pareto na kuweza kushindana na mataifa mengine kama vile Uchina.

Kinjuri amesema serikali ilikuwa imejitolea kuhakikisha kuwa sekta hiyo na ambayo ilikuwa ikileta mabilioni ya pesa kwa wakenya imefufuliwa na kuongeza kuwa serikali ya kitaifa itatoa shilingi milioni 45 kwa kaunti ya Nakuru ili kuweza kupanda mbegu za mmea huo zitakazopewa wakulima.

Naye gavana wa kaunti hiyo Lee Kinyanjui  amesema kuwa wametenga shilingi milioni 45 za kununua mbegu hizo na kuongeza serikali yake tayari imetoa shilingi milioni sabini za kuboresha fani mbali mbali za kilimo katika kaunti hiyo.

Wengine waliozungumza ni pamoja na katibu wa kudumu katika wizara hiyo Profesa Hamadi Mboga na mbunge wa Gilgil ambao wameelezea matumaini yao ya kuona kuwa sekta hiyo imefufuliwa.

About VANTAGE MUSIC RECORDS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.