Wakulima kutoka vijiji vinne kaunti
ndogo ya Gilgil wametishia kutolipa ushuru na ada zingine kwa kaunti ya Nakuru
kutokana na huduma hafifu zinazotolewa.
Wakizungumza baada ya kufanya
maandamano na kufunga barabara kuu ya Gilgil kuelekea Eburru, wakulima hao
kutoka vijiji vya Kamunyore, Gema Catholic, Kwa Gema na Nagum wamesema eneo
hilo limesahaulika kwa maendeleo kwa miaka mingi.
Kulingana na kiongozi wao Mary
Waithera, barabara za maeneo hayo hazijatengenezwa kwa muda wa miaka mitano
licha ya kuwa vijiji hivyo vimo kilomita kumi kutoka mji wa Gilgil.
Waithera ameongeza kuwa licha ya wao
kuahidiwa kuwa barabara hizo zitakarabatiwa hakuna kilichofanyika.
Naye Mary Nungari amesema eneo hilo
halina maji huku mtungi wa lita ishirini ukiwagharimu shilingi hamsini tukio
linalowafanya wao kuoga mara moja kwa wiki.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.