Ukusanyaji wa ushuru katika kaunti
ya Nakuru umefikia shilingi bilioni 2.8 katika kipindi cha matumizi ya fedha za
serikali cha mwaka uliopita.
Haya yamejiri huku serikali hiyo
ikipania kuweka mashine za kidijitali katika maeneo yote ya ukusanyaji fedha
kama njia moja ya kumaliza ufisadi na kuongezea mapato yako.
Kwa mujibu wa waziri wa fedha wa
kaunto hiyo Dkt Peter ketyenya, mwaka huu wanalenga kukusanya shilingi bilioni
2.6 na kuongeza walikuwa wakifanya mazungumzo na shirika la ukusanyaji ushuru
nchini KRA ili kuweza kubuni bodi sawia ya kaunti ya Nakuru.
Akizungumza wakati wa mkutano na
maafisaa wakuu wa idara ya fedha katika hoteli moja mjini Naivasha, Ketyenya
amesema kaunti hiyo ilikuwa ikipania kubuni sheria mpya itakayoangalia tena ada
zinazotozwa mashamba katika kila kaunti ndogo kumi na moja za kaunti hiyo.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.