Viongozi mjini Naivasha sasa
wamesema kuwa ongezeko la vituo vya kuwatunza watoto kwa muda maarufu kama Day
care centers na ambavyo havijaidhinishwa kisheria vimechangia pakubwa
kuongezeka kwa magonjwa kwa watoto eneo hilo.
Kulingana na aliyekuwa mwakilishi wa
wadi ya Lake View mjini Naivasha Simon Wanango, vituo hivyo havina na leseni
huku watoto wengi wanaopelekwa wakiadhiriwa na magonjwa tofauti.
Wanango amesema kuna haja ya
serikali kuchunguza vituo hivyo na kuongeza ni hivi majuzi ambapo mtoto mmoja
aliaga dunia baada ya kunyongwa na chakula katika kituo kimoja eneo la
Karagita.
Naye katibu wa muungano wa
wafanyikazi wa maua mjini Naivasha Ferdinand Juma amesema wafanyikazi wengi wa
kike wana waacha watoto wao vituoni na kuelekea kazini licha ya kutambua maeneo
wanakowaacha hayajaidhinishwa.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.