Viongozi wa kina mama katika baraza la viongozi wa jamii ya
Agikuyu (Thingira )wamewasuta wanasiasa kwa cheche za matusi dhidi ya rais
kufuatia juhudi zake za kusitisha ufisadi na kuunganisha wakenya nchini .
Wakiongozwa na Lucy Kibui na wambui Wakiromo baada ya
kikao chao cha majadiliano mjini Nakuru wamewataka wanasiasa kukoma
kuingiza siasa katika vita dhidi ya ufisadi na badala yake kumpongeza raisi kwa
hatua zake na kumtaka kamwe kutolegeza kamba.
Aidha Wametaja kuwa wanaunga mkono mpango wa
'building bridges' nchini wanaosema umefamikisha amani baina ya
jamii.
Kuhusiana na kura ya maoni wamesema wataunga mkongo mpangilio
wowote unaopelekea wote kushirikishwa kwa amani na maendeleo ya taifa
hili .
wakati uo huo wamemtaka rais Kenyatta kutangaza ugonjwa wa
saratani kuwa janga la kitaifakatika juhudi za kutafuta suluhu la kudumu.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.