|
Wauguzi wa madawa ya kiasili katika eneobunge la Eldama
Ravine sasa wanataka serikali kutambua sekta hiyo kikamilifu,na kuishirikisha
katika utafiti wa madawa na tiba za magonjwa mbali mbali kama vile saratani.
Wilson Kiragu ambaye ni mkaazi wa tarafa ya Torongo katika
eneobunge la Eldama Ravine amezungumza kwa niaba ya madaktari wa miti shamba wa
eneohilo,na anasema ugonjwa wa Saratani ambao umeibuka kuwa janga la kitaifa ,unaweza
kutibiwa kupitia kwa madawa ya kiasili.
Kiragu anataka serikali kuwekeza katika utafiti wa madawa hayo,kwa kushirikisha watafiti kutoka kwa vyuo vikuu vilivyoidhinishwa,ili
kulinda haki za umiliki kwa uvumbuzi wa dawa ya kutibu ugonjwa huo.
Katika kikao cha wanasayamsi wa kituo cha utafiti kuhusu
madawa KEMRI ,na kilichofanyika mwaka wa 2017 jijini Nairobi,wanasayansi kwenye
kikao hicho waliweza kutambua aina 20 ya mimea au miti za kiasili nchini
Kenya,na ambazo zina uwezo wa kutibu ugonjwa wa Saratani.
Katika kikao hicho cha siku tatu,Sabina Wangui Wachira wa
kituo cha utafiti kuhusu tiba za kiasili kwenye kituo hicho cha Kemri alidokeza
kwamba,madawa ya kutibu saratani hutengenezwa
kutokana na miti au mimea,kwa asilimia 60 .
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.