Powered by Blogger.

Header Ads


Tag:

VYAKULA VYENYE KEMIKALI NDIO CHANZO CHA SARATANI NCHINI ASEMA JOHN MUTUTHO



Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu kilimo John Mututho ameonya dhidi ya utumizi wa kemikali kwenye vyakula vinavyoliwa na wakenya.

Mututho amesema kuwa wakenya wengi walikuwa wakikula bidhaa zilizojaa kemikali na kuhatarisha maisha yao huku magonjwa kama vile saratani yakiendelea kuongezeka.

Akizungumza na wanahabari mjini Naivasha, Mututho amesema kuwa wakati ulikuwa umefika kwa Kenya kuangalia madhara yanayoletwa na vyakula vilivyotengenezwa kwa njia ya kisayansi maarufu kama GMO’s kwa madhumuni ya kuvipiga marufuku.

Huku akiomboleza na familia ya gavana wa Bomet Joyce Laboso na mbunge wa Kibra Ken Okoth, Mbunge huyo wa zamani wa Naivasha amesema mashirika husika ya serikali yalifaa kukagua vyema vyakual vinavyoletwa kutoka nchi za nje kama njia moja ya kulinda afya ya wakenya.

About VANTAGE MUSIC RECORDS

Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.