Muungano wa madakitari wa mifugo nchini KVA umeelezea wasi wasi
dhidi ya ongezeko la wanyama wanaochinjwa kwenye vichinjio wakiwa wagonjwa au wanaoletwa
wakiwa wameaga dunia.
Mwenyekiti wa muungano huo Dkt Samuel Kahariri amesema kuwa
mizoga ya wanyama hao ilikuwa ikipelekwa vichinjioni bila ya kujulikana huku
wahusika wakiweka nyama hiyo kemikali ili kuonekana kama ni safi
Akizungumza na wanahabari mjini Naivasha, Kahariri amesema
kulikuwa na haja ya serikali kuwaajiri wakaguzi wa nyama zaidi na kusema Kenya
kwa sasa ina vichinjio 2,500 lakini kuna wakaguzi mia tano pekee.
About VANTAGE MUSIC RECORDS
Hi, My Name is Hafeez. I am a webdesigner, blogspot developer and UI designer. I am a certified Themeforest top contributor and popular at JavaScript engineers. We have a team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.